Makaburi zaidi yavunjwa Timbuktu

Imebadilishwa: 23 Disemba, 2012 - Saa 16:27 GMT

Taarifa kutoka kaskazini mwa Mali zinaeleza kuwa wapiganaji wa Kiislamu wamevunja makaburi kadha ya kale katika mji wa Timbuktu.

Wapiganaji wax Kiislamu nje ya Timbuktu

Kiongozi mmoja wa wapiganaji hao ameliambia shirika la habari la Ufaransa kwamba makaburi yote mjini Timbuktu yatavunjwa, kwa sababu yanakwenda kinyume na Uislamu.

Kati ya mwaka huu makaburi kadha yalivunjwa katika mji huo ambao ni eneo la kuhifadhiwa kufuatana na Umoja wa Mataifa.

Makundi ya wapiganaji wa Kiislamu na mengineyo yaliteka eneo la kaskazini la Mali baada ya serikali ya taifa kupinduliwa awali mwaka huu.

Siku ya Alkhamisi Umoja wa Mataifa ulipitisha azimio kukubali kikosi cha nchi za Afrika kutumwa Mali.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.