Wanne watekwa nyara Nigeria

Imebadilishwa: 24 Disemba, 2012 - Saa 18:19 GMT
Ramani ya Nigeria

Ramani ya Nigeria

Maharamia wamewateka nyara mabaharia wanne baada ya kushambulia meli yao katika pwani na Nigeria.

Haya ni kwa mujibu wa shirika la kimataifa linalosimamia safari za meli IMB.

shirika la Habari la AP limesema kuwa mateka hao wote ni raia wa kigeni, watatu kutoka Italia.

watu wamejihami kwa bunduki walivamia meli hiyo katika eneo la Nigeri Delta lenya utajiri mkubwa wa mafuta, kabla ya kuwateka nyara wanne hao na kutoweka.

Utekaji nyara ni biashara inayohakikisha malipo ya juu nchini Nigeria na inakisiwa kugharimu mamilioni ya madola, katika taifa hilo ambalo kuzalisha kiasi kikubwa cha mafuta barani.

Idadi kubwa ya raia katika eneo hilo la Niger Delta ni masikini.

Wafanyakazi wa secta ya mafuta na raia wa kigeni ndio hulengwa zaidi na wahalifu hao kwa sababu wanalipwa kiasi kikubwa cha fedha kabla ya kuwaachilia.

Shirika hilo la IMB limesema meli hiyo ilitekwa nyara takriban kilomita 28 kutoka jimbo la Bayelsa.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.