Asilimia 60 waunga katiba Mpya-Misri

Imebadilishwa: 25 Disemba, 2012 - Saa 19:25 GMT
Tume ya uchaguzi ikitangaza matokeo Misri

Tume ya uchaguzi ikitangaza matokeo Misri

Tume ya uchaguzi nchini Misri imetangaza kuwa takriban asilimia sitini ya wapiga kura walioshiriki katika kura ya maoni kuhusu katiba mpya nchini Misri wameunga mkono hiyo.

Katika kura zote zilizopigwa asilimia 63.8% ya watu walipiga kura ya ndio katika duru zote za kura hiyo iliyofanika tarehe 15 na 22 mwezi huu.

Uchaguzi mkuu nchini humo sasa unatarajiwa kuandaliwa katika kipindi cha miezi miwili ijayo.

Wakosoaji wanasema katiba hiyo, ambayo imesababisha maandamano makubwa nchini humo, imehujumu mageuzi yaliyomuondoa madarakani rais Hosni Mubarak.

Mubarak aliondolewa madarakani mwezi Februari mwaka uliopita baada ya kuwa madarakani kwa muda wa miaka 30.

Raia wakiandamana Misri

Raia wakiandamana Misri

Lakini wafuasi wa rais Morsi, wengi wakiwa Waislamu wanasema katiba mpya itahakisha kuwepo kwa demokrasia na uthabiti nchini humo.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Cairo, rais wa Tume ya Uchaguzi nchini humo Samir Abul Maati amesema kuwa asilimia 32.9 ya wapiga kura Milioni 52 ndio waliojitokeza kupiga kura.

Bwana Maati, alipinga madai ya upinzani kuwa majaji bandia walisimamia baadhi ya vituo vya kupigia kura, moja kati ya malalamishi ya udanganyifu yaliyowasilisha na chama cha upinzani cha National Salvation Front.

Wapinzani wa rais Morsi wanamshutumu kwa kushinikiza kuwepo kwa kifungu fulani ambacho kinawapa Waislamu nafasi zaidi kuliko wengine na kuwa katiba hiyo hailindi haki na kina mama au Wakristo ambao ni asilimia 10 ya idadi watu wote nchini humo.egpt

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.