Askofu apinga ndoa ya wapenzi wa jinsi moja

Imebadilishwa: 25 Disemba, 2012 - Saa 13:00 GMT
Vincent Nichols

Vincent Nichols

Kiongozi wa Kanisa wa Katoliki nchini Uingereza amesema mpango wa serikali ya Uingereza kuhusu ndoa ya wapenzi wa jinsi moja ni jambo la aibu.

Askofu mkuu wa Jimbo wa Westminster Vincent Nichols ameiambia BBC kuwa serikali ya Uingereza haina wajibu wa kuhimiza ndoa ya wapenzi wa jinsia moja nchini Uingereza.

Katika hotuba yake wakati wa ibadi ya Krismasi, askofu Nichols alisema ndoa kati ya mwanamume na mwanamke inaashiria mapenzi ya Mungu.
Serikali ya Uinbereza inapanga kuruhusu ndoa ya wapenzi wa jinsi moja lakini imesema kuwa haitazishurutisha viongozi wa kidini kuongoza na kuidhinisha ndoa hizo.

Kwingineko, Askofu wa jimbo ya Centerbury anayeondoka, Rowan Williams amesema heshima na hadhi ya Kanisa la Kianglikana na nchini Uingereza, limeadhirika pakubwa kutokana na uamuzi wa hivi majuzi ambao ulipinga uteuzi wa kina mama kama askofu wa kanisa hilo.

Dr Williams anatarajiwa kustaafu kutoka wadhifa huo mwisho wa mwezi huu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.