Mwanawe Bhuto azindua kampeini

Imebadilishwa: 27 Disemba, 2012 - Saa 11:30 GMT
Bilawal Bhutto Zardari

Bilawal Bhutto Zardari

Mwanawe waziri mkuu wa Pakistan aliyeuawa, Benazir Bhutto, anazindua kuingia kwake kwenye siasa hii leo ikiwa ni maadhimisho ya mwaka wa tano tangu mamake kuuawa.

Bilawal Bhutto Zardari anatarajiwa kutangaza malengo yake kwa mara ya kwanza mbele ya maelfu ya wafuasi nyumbani mwao katika jimbo la Sindh.

Mamia ya maelfu ya wafuasi wa chama cha Pakistan Peoples Party walianza kufurika Larkana kabla ya siku hiyo kubwa.

Wanaharakati waliobeba picha za Benazir Bhutto, na babake, waziri Mkuu wa zamani Zulfiqar Ali Bhutto, wamekita kambi kote mjini humo.

Chama hicho tawala kinataka kutumia sherehe hiyo kuonyesha kuwa licha ya shutuma kuhusu utendakazi wake katika miaka mitano iliyopita, bado kina wafuasi wengi.

Hotuba kuu itatolewa namwanawe Bhutto, Bilawal Bhutto Zardari.

Itakuwa mara ya kwanza kwake kuhutubia mkutano wa maelfu ya wafuasi kuelezea maono ya chama hicho.

Aliteuliwa mwenyekiti wa chama hicho punde tuu baada ya kuuwawa kwa mamake na wapiganaji wa taliban mwaka wa 2007, lakini hajajitokeza hadharani kutokana na umri wake mdogo na kukosa uzoefu wa kisiasa.

Huku uchaguzi wa Bunge ukitarajiwa Pakistan katikati ya mwaka wa 2013, waliochoshwa na siasa za rais Zardari, wanamuangalia, kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 na aliyehitimu kutoka chuo cha Oxford, kufufua umaarufu wa chama hicho.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.