Watu 60 wafariki kwenye sherehe za mwaka mpya Ivory Coast

Imebadilishwa: 1 Januari, 2013 - Saa 12:58 GMT

Mavazi ya watu nwaliouawa kwenye msongamano mjini Abidjan

Zaidi ya watu sitini wamefariki na wengine mia mbili kujeruhiwa katika pwani ya Ivory coast katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya.

Kisa hicho kilitokea kufuatia msongamano wa watu wakati wa sherehe hizo, za kuukaribishwa mwaka mpya wa 2013.

Vyombo vya habari vya taifa hilo vinasema tukio hilo lilitokea mapema alfajiri katika jiji kuu la Abijdan.

Inasemekana kuwa watu hao walikuwa wakishuhudia maonyesho ya fataki katika uwanja wa michezo.

Wengi waliofariki ni watoto kati ya miaka minane hadi kumi na mitano.

Hata hivyo haijulikani kilichosababisha msongamano huo.

Ajali hiyo ilitokea katia uwanja wa michezo wa Felix Houphouet Boign, ambao una ukumbwa wa kuruhusu mashabiuki elfu sitini na tano wa soka na ulipewa jina hilo kama heshima ya rais wa kwanza wa nchi hiyo.

Kabla ya ajali hiyo uwanja huo uliandaa maonyesho ya muziki iliyohudhuriwa na mwana muziki kutoka Marekani Chris Brown.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.