Viongozi wa M23 wawekewa vikwazo na UM

Imebadilishwa: 1 Januari, 2013 - Saa 13:53 GMT

Mpiganaji wa M23 akiwa na chombo cha mawasiliano

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limewawekea vikwazo viongozi wa kundi la waasi wa M23 nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Chini ya sheria hiyo, mali ya watu watakaohusishwa na kundi hilo itapigwa tanji na kuzuiliwa kusafiri katika mataifa ya nje.

Umoja wa mataifa ulichukua hatua kama hiyo dhidi ya viongozi wa waasi wa FDLR.

Kundi hilo la M23 lililoundwa na wanajeshi waasi,waliuteka mji wa Goma, Mashariki mwa Congo karibu na mpaka wa nchi hiyo na Rwanda, kutoka kwa wanajeshi wa serikali na wale wa kutunza amani wa Umoja wa Mataifa.

Waasi wa M23 washurutishwa kuondoka Goma

Wapiganaji wa Waasi wa M23

Lakini kufuatia shutuma kutoka kwa jamii ya kimataifa wapiganaji hao walikubali kuondoka kutoka mjini humo mwezi uliopita.

Tangazo hilo limetolewa mkesha wa siku ya mwaka mpya siku moja tu kabla ya Rwanda kujiunga kuwa mwanachama wa baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka miwili.

Umoja wa Mataifa na Serikali ya Congo, zimeishutumu serikali za Rwanda na Uganda kwa kuwaunga mkono wapiganaji hao wa waasi, madai ambayo yamepingwa vikali za serikali hizo mbili.

Rwanda inatuhumiwa kuunga mkono makundi ya waasi Mashariki mwa Congo, kama njia moja ya kupambana na wapiganaji wa waasi wa Kihutu ambao walitoroka nchini humo baada ya mauaji ya kimbari miaka ya tisini.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.