Bunge la Senate lapitisha mswada wa Obama

Imebadilishwa: 1 Januari, 2013 - Saa 12:43 GMT
Rais Obama

Rais Obama

Rais wa Marekani Barrack Obama, amewataka wabunge wa bunge la wawakilishi kupitisha maazimio yaliopitishwa na bunge la Senate kuhusu sera mpya ya uchumi bila kusita.

Bwana Obama, amesema kuwa makubaliano hayo yanawaokoa asili mia sabini ya Wamarekani dhidi kupandishiwa ushuru na pia yataimarisha uchumi uchumi waa taifa hilo.

Rais Obama, amesema kuwa kwa mara ya kwanza wanaomiliki mabilioni na mamilioni ya fedha watalazimika kulipa ushuru unaohitajika kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka ishirini iliyopita.

Wabunge wa chama cha Republican, wamesema kuwa watahitaji muda zaidi kusoma mapendekezo hayo.

Hata hivyo wantarajiwa kupiga kura baadaye hivi leo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.