Kesi dhidi ya Cecil yafutiliwa mbali Uganda

Imebadilishwa: 2 Januari, 2013 - Saa 18:44 GMT

David Cecil akiwa korokoroni

Mahakama moja nchini Uganda, imefutilia mbali kesi dhidi ya mwandishi mmoja wa michezo ya tamthilia, David Cecil, ambaye alikuwa akikabiliwa na shtaka la kuonyesha mchezo kuhusu hali ya wapenzi wa jinsia moja, katika mji mkuu wa nchi hiyo Kampala.

Bwana Cecil, alikabiliwa na tuhuma za kukiuka sheria kwa makusudi.

Bwana Cecil ameiambia BBC, kuwa kesi hiyo ilifutiliwa mbali kutokana na kile alichokitaja kama ukosefu wa ushahidi wa kutosha dhidi yake.

Mshukiwa huyo alikamatwa mwezi Septemba, kwa kukiuka sheria za hiyo kwa kuonyesha mchezo huo bila kibali wenye maudhui ''The River and the Mountain''

Mapenzi ya jinsia moja imeharamishwa nchini Uganda.

Bunge la nchi hiyo linajadili uwezekano kwa kuimarisha adhabu ya wale watakaopatikana wakijihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Rais wa Uganda akikagua gwaride la kijeshi

Ikiwa angelipatikana na hatia Bwana Cecil, angelihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani.

Alipigwa faini ya laki tano pesa za Uganda, sawa na dola mia mbili za Marekani.

Akiongea muda mfupi baada ya kesi dhidi yake kufutiliwa mbali Bwana Cecil alisema kuwa amefurahishwa na uamuzi huo, licha ya hofu kuwa huenda akafunguliwa mashtaka mengine.

Wakati huo huo, Wabunge wa Uganda, wanajaribu kuitisha Bunge likatishe kipindi cha mapumziko ili lijadili kukamatwa kwa baadhi ya wabunge kuhusiana na kifo cha mbunge mwanamke wa wilaya ya Butaleja, mashariki mwa Uganda, wiki mbili zilizopita.

Kifo hicho kimezusha hofu na mabishano ya kikatiba baina ya Rais Yoweri Museveni na wabunge.

Ili kufanikisha ombi hilo, inapasa kwa uchache wabunge 125 walitie sahihi na kisha kulifikisha kwa Spika, mwenye uwezo wa kulirudisha Bunge.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.