Misri yabadilisha baraza la mawaziri

Imebadilishwa: 6 Januari, 2013 - Saa 14:51 GMT
Sarafu ya Misri imepoteza thamani

Mawaziri sita wameapishwa nchini Misri katika mabadiliko ya mwanzo ya baraza la mawaziri tangu katiba mpya kukubaliwa.

Serikali sasa ina mawaziri wepya wa fedha na mashauri ya ndani ya nchi, wakati serikali inajaribu kuimarisha uchumi uliozorota na sarafu iliyoporomoka.

Waziri mpya wa fedha, El-Morsy El-Sayed Hegazy, amekariri kuwa Misri inataka kukubaliana na IMF, ipewe mkopo wa dola bilioni nne na laki nane milioni, ambao ulicheleweshwa kwa sababu ya msuko-suko wa kisiasa nchini humo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.