Nelson Mandela hajambo

Imebadilishwa: 6 Januari, 2013 - Saa 15:58 GMT
Mandela

Serikali ya Afrika Kusini inasema rais wa zamani wa nchi hiyo, Nelson Mandela, hajambo baada ya ugonjwa wa mapafu na upasuaji wa kutoa mawe kwenye kibofu nyongo.

Alikuwa hospitali kwa majuma kadha mwezi wa Disemba.

Taarifa rasmi iliwanukuu madaktari waliomtibu wakisema kuwa Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 94, amepata nafuu na afya yake inazidi kutengenea.

Rais huyo amebaki nyumbani kwake mjini Johannesburg tangu alipotoka hospitali siku 11 zilizopita.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.