Rais Chavez hataapishwa kwa sasa

Imebadilishwa: 9 Januari, 2013 - Saa 08:15 GMT

Rais Hugo Chavez alishinda uchaguzi mwaka jana na sasa atatawala kwa muhula wa nne

Bunge la venezuela limepiga kura ya kuidhinisha kuhakhirishwa kwa shughuli ya kuapishwa kwa raisi wa venezuela Hugo Chavez kutawala kwa muhula mpya.

Sherehe hizo zilitarajiwa kufanyika hapo keshio siku ya Alhamisi.

Manaibu walipiga kura kumpa rais muda anaohitaji kuweza kupata nafuu kutokana na upasuaji aliofanyiwa wa saratani mwezi jana.

Makamu wa raisi Nicolas Maduro amesema kuwa rais Chavez hatoweza kusafiri hadi Venezuela kwa sherehe hiyo ya kuapishwa kutokana na madakatari wake nchini Cuba kusema kuwa haruhusiwi kusafiri .

Upinzani unasema kuwa Bwana Chavez anapaswa kusemekana kuwa hawezi kazi tena na hivyo spika wa bunge kuchukua nafasi ya rais wa mpito.

Bwana Chavez, ambaye amakuea mamlakani tangu mwaka 1999, alichaguliwa kwa muhula wake wa nne mamlakani katika uchaguzi uliofanyika mwezi Oktoba.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.