AU yaomba msaada wa NATO Mali

Imebadilishwa: 9 Januari, 2013 - Saa 15:07 GMT

Wapiganaji wa kiisilamu nchini Mali

Mwenyekiti wa Muungano wa Afrika, Thomas Boni Yayi, ametoa wito wa kutuma vikosi kusaidia wanajeshi kupambana na makundi ya wapiganaji nchini Mali.

Wapiganaji hao ambao wanajumuisha wale wa Tuareg, wameteka eneo la Kaskazini mwa nchi.

''Mzozo wa Mali ulikuwa kitendawili cha kimataifa na NATO inapaswa kusaidia kama ilivyo saidia Afrghanistan,'' alisema Thomas Boni Yayi

''Hata hivyo, harakati dhidi ya wapiganaji hao zinapaswa kuongozwa na kikosi cha Afrika,'' aliongeza kusema bwana Yayi.

Mwezi jana Umoja wa Mataifa uliidhinisha mipango ya kutuma takriban kikosi cha wanajeshi elfu tatu nchini Mali.

''Bila shaka tuna wasiwasi kuhusu hali na hofu ya kuendelea kuwepo makundi ya kigaidi katika eneo hilo , inaleta wasiwasi kwa kila mtu kimataifa''

Maafisa wa UN wanasema kuwa hawakutarajia wanajeshi hao kutumwa huko kabla ya mwezi Septemba.

Bwana Yayi, ambaye ni rais wa Benin,alitoa wito wake baada ya mazungumzo na waziri mkuu wa Canada Stephen Harper mjini Ottawa.

"NATO inapaswa kuchukua jukumu lake katika mzozo huu, na kwamba kikosi cha Afrika kitatoa mwongozo, sawa tu na hali ilivyokuwa nchini Afghanistan,''

Wanachama kadhaa wa NATO ikiwemo, Marekani na Ufaransa, wako tayari,kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Afrika watakaoshiriki katika harakati hizi za kumaliza uasi, ingawa hawajajitolea kutuma vikosi.

Bwana Harper alisema kuwa Canada , ambayo ni mwanachama wa , Nato, haijatafakari zaidi kuhusu kujihusisha kijeshi nchini Mali.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.