Hali ya Kibinadamu yazorota zaidi Sudan

Imebadilishwa: 9 Januari, 2013 - Saa 09:21 GMT

Wanawake katika mkoa wa Kordofan Kusini wakisubiri msaada

Umoja wa mataifa umeonya kuhusu kuendelea kudorora kwa hali ya kibinadamu katika maeneo yanayokabiliwa na mizozo katika mikoa ya Kordofan ya kusini na Blue Nile nchini Sudan.

Inaarifiwa kuwa watu wanakufa na maelfu wakilazimika kula mizizi na majani ya miti ili waweze kuishi.

Umoja wa mataifa ulisema kuwa watu laki saba wameathiriwa katika maeneo hayo.

Afisaa mkuu wa misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, John Ging, alisema kuwa serikali na Sudan na waasi wamekosa kujitolea kisiasa kuokoa hali na ndio sababu kuu ya masaibu ya wenyeji.

Alisema kuwa juhudi za mwaka mmoja kuweza kuingia katika eneo hilo zilikosa kufaulu.

Mkuu huyo alisema kuwa hali ya kibinadamu ya watu ni mbaya mno, na kwamba ikiwa hali haitaweza kunusuriwa basi, watu wataendelea kuteseka na hata kufariki.

Aliongeza kuwa huenda watu wakalazimika kutoroka na kukimbilia nchini Ethiopia.

Bwana Ging alisema mashirika ya kibinadamu yanakabiliwa na hali ngumu na kwamba yako tayari kupeleka chakula na dawa kwa waathiriwa.

Mapigano kati ya sudan na makundi ya waasi ndiyo inasekena akuchochea mzozo huu

Pia alitoa ombi kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa kusaidia kuokoa hali.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa,Susan Rice, aliitikia kuwa pande hizo mbili zinazo zozana, zinapaswa kulaumiwa lakini serikali ya Khartoum ndiyo inapaswa kulaumiwa pakubwa.

Hata hivyo baadhi ya wanachama wa baraza la usalama wameonekana kuitetea Khartoum zaidi wakisma ina haki ya kujilinda dhidi ya makundi ya waasi.

Aliongeza kuwa Marekani inaunga mkono kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya pande zinazozozana kufuatia azimio la mwaka jana ambalo lilitishia kuziwekea vikwazo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.