Waasi Jamuhuri ya Afrika ya Kati wasitisha vita

Imebadilishwa: 11 Januari, 2013 - Saa 10:28 GMT

Kiongozi wa waasi wa Seleka

Waasi wanaopambana na serikali katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, wanasema kuwa wamekubaliana kusitisha mapigano kwa wiki moja baada ya mazungumzo ya amani nchini Gabon.

Waasi wanasema kuwa wanataka wanajeshi wa Afrika Kusini waondoke nchini humo na pia serikali iwaachilie wafungwa wa kisiasa ili waweze kuafikia mwafaka wa pamoja.

Waasi hao wa 'Seleka' walidhibiti maeneo ya Kaskazini na Mashariki kwa CAR katika kipindi cha wiki nne kuanzia Disema mwaka jana.

Wanamtuhumu rais Francois Bozize kwa kukiuka mikataba kadhaa ya amani ambayo walitia saini.

''Tutakubaliana kimsingi kutopigana kwa wiki moja'' alisema msemaji wa kundi hilo, Florian Ndjadder.

Aliongeza kuwa mwafaka utaweza kuruhusu waasi kuona ikiwa serikali itaweza kujitolea kupata suluhu kwa mzozo huu na kutimiza matakwa yao.

Waasi hao ambao wamekuwa wakimtaka rais kujiuzulu, pia walisema kuwa wanataka waziri mkuu mpya kuteuliwa kutoka kwa upinzani na hata kutoa madai zaidi.

Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Francois Bozize akiwahutubia waandishi wa habari

" Mamluki hao kutoka Afrika Kusini lazima waondoke Jamuhuri ya Afrika ya Kati, wafungwa wa kisiasa lazima waachiliwe bila vikwazo wakati huohuo,'' alisema bwana Ndjadder.

Afrika Kusini imeanza kutuma wanajeshi 400 kusaidia kudhibiti hali katika Jamuhuri ya Afrika ya kati. Wanajeshi kutoka nchi jirani pia wameweza kutumwa huko. Ufaransa na Marekani wamekataa ombi la serikali kusaidia katika kupambana na waasi hao.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.