Waasi wauteka uwanja wa ndege Syria

Imebadilishwa: 11 Januari, 2013 - Saa 11:30 GMT

Waasi wa Syria wanakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa jeshi

Waasi wameripotiwa kutwa udhibiti wa uwanja muhimu wa ndege wa kijeshi, Kaskazini Magharibi mwa Syria, baada ya wiki kadhaa za mapigano na wanajeshi wa serikali.

Wanaharakati wa upinzani wanasema kuwa waasi wa Free Syrian Army, wanadhibiti uwanja wa ndege wa Taftanaz. Waasi hao wameoneka wakiwa nje ya uwanja huo kwenye kanda ya video iliyoonyeshwa kwenye mtandao.

Ndege za jeshi zilizoko katika eneo hilo zimetumika katika mapambano dhidi ya waasi hao, katika ngome zao.

Wakati huohuo, maafisa wakuu nchini Urusi na Marekani, watahudhuria mkutano na mjumbe maalum wa umoja wa mataifa nchini Syria, Lakhdar Brahimi.

Wanatarajiwa kujadili ambavyo wataweza kuafikia mpango wa amani uliopendekezwa na vuguvugu la 'Action Group for Syria' mwezi Juni , lakini duru zinasema kuwa huenda ikawa vigumu kuafikia chochote kwa njia ya kidiplomasia.

Mpango huo umeitisha mara moja usitishwaji wa ghasia na kuundwa kwa serikali ya mpito, ambayo itajumuisha maafisa wanaohudumu chini ya serikali ya Bashar al-Assad pamoja na wanachama wa 'upinzani .

Urusi na Marekani zinatofautiana kuhusu ikiwa bwana Assad anapaswa kuondoka mamlakani.

Mnamo siku ya Alhamisi, serikali ya Urusi, ilimtuhumu bwana Brahimi kwa kuwa na mapendeleo kufuatia matamshi aliyotoa ya kumkashifu rais Assad wakati wa mahojiano kwenye BBC.

Alisema kuwa watu wanahisi miaka uarobaini ni muda mrefu sana kwa familia moja kutawala nchi.

Kulingana na ripoti za umoja wa mataifa, zaidi ya watu 60,000 wameuawa tangu harakati za mapinduzi dhidi ya utawala wa Assad kuanza mwezi Machi mwaka 2011.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.