Hewa ya Beijing ni mbaya sana

Imebadilishwa: 12 Januari, 2013 - Saa 17:27 GMT

Kuchafuka kwa hali ya hewa katika mji mkuu wa uchina, Beijing, kumefikia kiwango kibaya kabisa kuwahi kutokea kwa miaka kadha.

Beijing

Vipimo rasmi vya uharibifu wa hewa vimepindukia kiwango ambapo watoto wote pamoja na wazee huambiwa wasitoke nje.

Mwandishi wa BBC mjini Beijing anasema kwa siku kadha sasa kumekuwa na ukungu mzito, na hewa ina ladha ya moshi wa makaa na magari.

Hata ndani ya nyumba kumetanda.

Moshi kama huo huleta shida za kupumua na kuzidisha idadi ya watu wanaokufa kwa sababu ya saratani ya mapafu na ugonjwa wa moyo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.