Mugabe na Tsvangirai wakubaliana kuhusu katiba

Imebadilishwa: 18 Januari, 2013 - Saa 13:29 GMT

Rais Mugabe anataka kuwania urais baada ya kuwa mamlakani tangu mwaka 1980

Viongozi mahasimu nchini Zimbabwe wamesema kuwa wameafikia makubaliano kuhusu katiba mpya ya nchi .

Makubaliano haya yanaondoa kikwazo kikubwa katika kuandaliwa kwa uchaguzi mkuu nchini humo.

Mkataba uliafikiwa katikammazungumzo yaliyowahusisha rais Robert Mugabe na waziri mkuu Morgan Tsvangirai.

Bwana Tsvangirai alisema kuwa safari ndefu imekamilika wakati rais Mugabae naya eakisema kuwa ana furaha hatimaye makubaliano yameafikiwa.

Waziri mkuu alikuwa ameweka kikwazo cha sherti kupatikana katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika baadaye mwaka huu.

Chama chake waziri mkuu MDC na kila cha rais Mugabe, vilikubaliana kuungana baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2008 ambao ulikumbwa na vurugu pamoja na madai ya wizi wa kura.

Mwandishi wa BBC mjini Harare anasema kuwa maelezo kuhusu makubaliano bado hayajatangazwa hadharani lakini inafahamika kuwa mamlaka ya rais yatapunguzwa.

Na hii ni mojawapo ya matakwa ya chama cha MDC.

Mugabe ambaye ana umri wa miaka 88 na ambaye anatarajiwa kugombea urais kwa muhula mwingine, alikuwa mwingi wa furaha alipohutubia mkutano wa waandishi wa habari katika makao yake.

"tuna furaha kuu kusema kuwa tumeweza kukubaliana na pande zote zinakubaliana kuwa bado tuna safari ndefu'' alisema Mugabe.

''Bwana Tsvangirai aliongeza kuwa katiba itakuwa mkataba kati ya serikali na wananchi. Sio kuhusu watu binafsi ''Nina uhakika kuwa hii itakuwa stakabadhi ya kudumu.'' aliongeza rais Mugabe.

Alisema kuwa katiba hiyo imesalia sasa kupigiwa kura ya maamuzi. Pindi itakapokubalika na wapiga kura , ndipo uchaguzi utatangazwa.

Rais Mugabe amekuwa mamlakani tangu mwaka 1980 na anatarajiwa kugombea urais na waziri mkuu Tsvangirai

Duru katika mchakato wa kuunda katiba zilisema kuwa tofauti kuhusu mfumo wa serikali pia ziliweza kutatuliwa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.