ECOWAS yataka tuma wanajeshi Mali haraka

Imebadilishwa: 19 Januari, 2013 - Saa 16:37 GMT

Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi wanakutana nchini Ivory Coast kwa kikao maalumu kuhusu Mali.

Ndege za Ufaransa nchini Mali

Katika kikao chao cha faragha wametoa wito wa msaada zaidi wa kimataifa katika kile walichoita vita dhidi ya ugaidi.

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, ambaye anahudhuria mkutano huo, ametoa wito wa wanajeshi wa Afrika kutumwa Mali haraka na kuanza kutumika.

Akihutubia mkutano wa nchi za Afrika Magharibi, Waziri wa Mashauri ya nchi za Nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, alisema jambo muhimu ni kufanya haraka kutuma wanajeshi Mali.

Alithibitisha kuwa Ufaransa itaongoza ujumbe wa Ulaya mwezi ujao ili kusaidia kulifunza na kulijenga tena jeshi la Mali.

Bwana Fabius piya aliwasihi washirika wa kimataifa wa Afrika wasaidie kwa usafiri na fedha.

Alieleza kuwa mkutano wa wafadhili utafanywa mjini Addis Ababa mwisho wa mwezi, na alisema mkutano huo utakuwa muhimu kushughulikia mahitaji ya Mali na kanda hiyo.

Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast, ambaye ndiye mwenyeji wa mkutano wa Abidjan, alisema wakati umefika kwa mataifa na mashirika makuu kuonesha mshikamano zaidi na kujitolea kuisaidia Afrika na Ufaransa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.