ECOWAS yaomba isaidiwe Mali

Imebadilishwa: 20 Januari, 2013 - Saa 15:39 GMT

Viongozi wa nchi za Afrika magharibi wameomba msaada wa kimataifa kugharimia majeshi yao kuingilia kati nchini Mali.

Wanajeshi wa Ufaransa nchini Mali

Walisema hayo kwenye mkutano unaofanywa Abidjan, Ivory Coast.

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, ambaye amehudhuria mkutano huo, ameshikilia kuwa majeshi ya Afrika yatashika uongozi wa operesheni za kijeshi nchini Mali katika majuma yajayo.

Nchi kadha za Afrika Magharibi zimeahidi kujitolea kwa wanajeshi ili kulisaidia jeshi la Ufaransa katika mapambano yake dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu, lakini nchi hizo zina shida za usafiri na fedha na hivo zinaweza kuchelewa kutuma wanajeshi wao Mali.

Hata hivo, Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, amesisitiza kuwa majeshi ya Afrika yatachukua nafasi ya Ufaransa katika majuma tu yajayo.

Lakini uwezo mdogo wa wanajeshi wa Afrika Magharibi kushiriki kwenye vita kaskazini mwa Mali huenda ukaifanya Ufaransa ilazimike kubaki vitani kwa miezi kadha ijayo.

Wanabalozi wa mataifa ya magharibi wanasema kuwa kisa cha wageni kutekwa nchini Algeria, kimeyafanya mataifa makuu kuamini kuwa lazima yapambane na makundi ya wapiganaji wa Kiislamu yalioko kaskazini mwa Mali.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.