Mateso ya wafungwa yakithiri Afghanistan

Imebadilishwa: 21 Januari, 2013 - Saa 13:16 GMT

Mojawapo ya magereza katika mkoa wa Kandahar

Umoja wa Mataifa umesema kuwa visa vya mateso katika magereza ya Afghanistan vimekithiri licha ya mapandekezo yake katika ripoti iliyotolewa mwaka 2011

Zaidi ya wafungwa 635 waliohojiwa na wachunguzi wa Umoja wa mataifa walisema walidhulumiwa au kuteswa.

Serikali ya Afghanistan hata hivyo inasema kuwa madai hayo yameongezwa chumvi. Jeshi la NATO nchini humo limeakhirisha shughuli ya kuwahamisha wafungwa katika baadhi ya magereza yaliyotajwa katika ripoti hiyo.

Ripoti hiyo iliangazia zaidi vituo vya kitaifa na vile vya mikoani kati ya mwezi Okotoba mwaka 2011 na Oktoba mwaka 2012.

Kosa la kutojali.

Kulingana na ripoti hiyo, kuna mbinu kadhaa za mateso ambazo hutumiwa ikiwemo kuchapwa kwa wafungwa, vitisho vya kuuawa na dhulma za kimapnenzi.

Baadhi walipigwa kwa nyaya za stima, ili kusema ukweli, wakati polisi wakitafuta taarifa.

Idadi ya visa vilivyoripotiwa wakati wafungwa wakiwa mikononi mwa polisi viliongezeka kutoka asilimia
35 hadi 43 ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa,ingawa serikali ilikuwa imetekeleza baadhi ya mapendekezo ya ripoti ya mwaka 2011, iligunduliwa kuwa hatua hazikuchukulia katika kuwakamata waliokuwa wanafanya mateso.

Uchunguzi haukufanywa kuweza kuwakamata au kuwafungulia mashtaka washukiwa

Rais wa Afghan, Hamid Karzai, amesisitiza kuwa swala la wafungwa linafungamana na uhuru wa Afghanistan na ameitaka Marekani kuikabidhi serikali yake wafungwa inaowazuilia

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.