Raia 37 wa kigeni waliuawa Algeria

Imebadilishwa: 21 Januari, 2013 - Saa 15:39 GMT

Wanajeshi wa Algeria wadhibiti uwanja wa Ndege mjini Ain Amenas

Waziri mkuu wa Algeria Abdelek Sellal amesema mateka 37 wa kigeni kutoka nchi 8 za kigeni waliuawa katika makabiliano ya watekaji nyara na jeshi.

Katika taarifa yake wazieri mkuu alisema kuwa raia mmoja wa Canada ni miongoni mwa wapiganaji walioteka kiwanda cha gesi na kuwakamata mateka.

Alisema kuwa watekaji nyara 29 waliuawa na wengine watatu walikamatwa wakiwa hai.

Tukio hilo lilifika kikomo siku ya Jumapili . Inaaminika mateka zaidi ya 45 wakiemo raia wa Algeria waliuawa.

Wanajeshi wanaendelea na upekuzi katika eneo kulipotokea utekaji nyara katika kiwanda cha mafuta cha Amenas. Ndani ya kiwanda hicho zaidi ya maiti ishirini zilizoteketea kiasi cha kutoweza kutambulika zilipatikana.

Taarifa zaidi zinaarifu kuwa Maiti za mateka kutoka Japan, Norway, Uingereza, Marekani na Malaysia bado hazijatambuliwa huku maafisa wa usalama wakisema kuwa watekaji nyara watano tayari walithibitishwa kuuawa na wapiganaji.

Takriban mateka 48 wameaminika kuuawa katika siku nne za sokomoko kwenye kiwanda cha gesi nchini Algeria.

Wanamgambo 5 inaarifiwa walikamatwa hiyoJumapili

Maafisa wa utawala awali walisema Jumamosi kuwa watekaji nyara 32 waliuawa.

Hata hivyo makomando waliweza kumaliza vurugu hilo siku ya Jumamosi. Maafifa walisema kuwa idadi kamili ya watu waliofariki itatolewa baadaye.

Jeshi lililazimika kufanya operesheni hiyo baada ya wanamgambo hao kuanza kuwaua mateka.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron na rais wa Marekani, Barack Obama, wamelaumu magaidi kwa kusababisha vifo vya mateka.

Kiongozi wa wapiganaji wa kiisilamu Algeria Mokhtar Belmokhtar

Kingozi wa wapiganaji hao, Mokhtar Belmokhtar, alisema kuwa wako tayari kufanya mazungumao na serikali ya Algeria lakini sharti wakome kushambulia wapiganaji wa kiisilamu nchini Mali.

Na Jumapili, waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian, alitaja kitendo cha wanamgambo hao kama kitendo cha vita.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.