Mlinzi mkuu wa Joseph Kony auawa

Imebadilishwa: 21 Januari, 2013 - Saa 15:08 GMT

Joseph Kony

Jeshi la Uganda limesema wanajeshi wake katika Jamhuri ya Afrika ya kati, wamemuua mlinzi mkuu wa Kiongozi wa waasi wa Lord's Resistance Army, LRA Joseph Kony.

Msemaji wa Jeshi Felix Kulayigye amesema mlinzi huyo anayetambulika kama Binani, aliuawa katika ufyatulianaji wa risasi kaskazini mwa Mji wa Djema.

Binani anaripotiwa kuwa miongoni mwa viongozi wakuu wa kundi hilo la waasi.

Kikosi cha wanajeshi wa muungano wa Afrika wakishirikiana na washauri kutoka Marekani wanawasaka vikali wapiganaji wa LRA wanaoendesha shughuli zao katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Sudan kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kony anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.