Wanajeshi wa Ufaransa wadhibiti Diablay

Imebadilishwa: 21 Januari, 2013 - Saa 12:00 GMT

Harakati za jeshi la kigeni nchini Mali

Wanajeshi wa Ufaransa na wa Mali, wameingia katikati mwa mji wa Diabaly, bila ya makabiliano yoyote na wapiganaji wa kiisilamu.

Msururu wa magari 30 ya kijeshi yaliyokuwa yamewabba wanajeshi 200 wa Mali na Ufaransa, yalionekana yakielekea mjini humo.

Wapiganaji walitoroka Ijumaa baada ya mji huo kushambuliwa kwa ndege za kijeshi

Ufaransa ilianza operesheni yake ya kijeshi dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu nchini Mali wiki moja iliyopita ili kujaribu kuwaondoa wapiganaji wanaodhibiti Kaskazini mwa Mali.

Jeshi la Ufaransa linanuia kuweza kudhibiti eneo hilo kikamilifu kutoka kwa wapiganaji wa kiisilamu. Hii ni kwa mujibu wa waziri wa ulinzi wa Ufaransa,Jean-Yves Le Drian.

"hatutaondoka bila ya kuwafurusha kabisa wapiganaji hao, '' waziri aliambia vyombo vya habari.

Ufaransa imetuma takriban wanajeshi 2,000 kusaidia Mali kupambana na wapiganaji hao wa kiisilamu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.