Eritrea:Majeshi yapelekwa Asmara

Imebadilishwa: 21 Januari, 2013 - Saa 15:41 GMT

Rais Isaias Afewerki ametawala Eritrea tangu mwaka 1993 ambapo nchi hiyo ilijipatia uhuru wake

Ripoti kutoka nchini Eritrea zinasema kuwa kikosi cha wanajeshi 200 wakitumia vifaru wamezingira wizara ya habari na mawasiliano katika mji mkuu Asmara.

Kituo cha televisheni ya taifa kimezimwa katika kile ambacho kinaaminika kuwa jaribio la mapinduzi.

Kwa sasa mji unaarifiwa kutulia na hakuna milio ya risasi imesikika.

Serikali ya Eritrea imekuwa ikituhumiwa na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, kama mojawapo ya nchi ambazo zinakandamiza sana raia wake.

Mitandao muhimu ya serikali pamoja na matangazo ya vyombo vya habari vya chama tawala, vyote vimevamiwa huku mtandao rasmi wa chama tawala, PFDJ ukiwa umefungwa.

Taarifa imesomwa kupitia televisheini na redio ya taifa ikitaka katiba ya nchi ya mwaka 1997 kutekelezwa.

Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza, imesema kuwa ilipokea taarifa za kutatanisha kuhusu jeshi mjini Asmara na kuelezea kuwa vituo vya televisheni na redio ya taifa vimefungwa.

Rais Isaias Afewerki ametawala nchi hiyo tangu ipate uhuru wake kutoka kwa Ethiopia mwaka 1993.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.