Nafasi za kazi zadidimia duniani

Imebadilishwa: 22 Januari, 2013 - Saa 07:57 GMT

Watu wengi Ulaya wamelazimika kukaa bila ajira kufuatia mipango ya serikali kuwaachisha kazi ili kupunguza matumizi

Shirika la kimataifa la wafanyakazi, limesema kuwa viwango vya ukosefu wa ajira vimeongozeka sana kote duniani hasa hasa kufuatia mipango ya serikali kuwafuta kazi wafanyakazi ili kupunguza matumizi ya pesa za serikali.

Inaarifiwa kuwa huenda mipango hiyo ikaendelea kukosesha watu wengi kazi ikiwa itaendelea kutekelezwa.

Viwango vya ukosefu wa ajira duniani vilipanda kwa zaidi ya milioni nne mwaka jana.

Hii ilikuwa asilimia mbili ya wafanyakazi waliokuwa wameajiriwa.

Watu walio chini ya umri wa miaka 24 nduio waliothirika zaidi kuliko wote.

Shirika hilo linasema kuwa takriban asilimia 13 ya vijana hao ,hawana ajira , hawasomi na wala hawako kwenye mafunzo yoyote.

Aidha ILO limeonya kuwa viwango vya ukosefu wa muda mrefu wa nafasi za kazi, vinaongezeka huku zaidi ya thuluthi moja ya watu barani Ulaya wakiwa hawana kazi kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.