Obama tayari kwa muhula wa pili

Imebadilishwa: 22 Januari, 2013 - Saa 13:14 GMT

Obama tayari kwa muhula wa pili

Rais wa Marekani, Barack Obama, wamewaambia wananchi wa Marekani kutumia fursa hii kujiimarisha katika hotuba aliyoitoa mjini Washington DC wakati wa sherehe za kumuapishwa kwa muhula wake wa pili.

Aliwasihi wamarekani kuungana na kuwa na umoja wa kisiasa wakati akielezea umuhimu wa kufurahia haki uhamiaji, mapenzi ya jisnia moja na vita dhidi ya tabia nchi au athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Bwana Obama, mwenye umri wa miaka 51, na ambaye ni rais wa 44 wa Marekani, aliapishwa kwa muhula wake wa pili na jaji mkuu
John Roberts.

Maelfu ya watu walisongamana katika sherehe za kuapishwa kwa Obama mjini DC.

Marais wa zamani, Bill Clinton na Jimmy Carter, pamoja na mamia ya maseneta , wabunge wa Congress walihudhuria sherehe hizo.

Obama alitoa ruwaza yake ya miaka minne ijayo, na kurejelea kusema kuwa safari ingali haijakamilika.

Obama na mkewe Michelle wakisherehekea

Aligusia baadhi ya maswala yanayowakera wapinzani wake na hasa wale ambao hawakumpigia kura.

''Kizazi hiki cha Marekani, kimekabiliwa na mambo mbali mbali na ambayo yaliwawezesha kuonyesha ujasiri wao. Miaka kumi ya vita sasa inakamilika. Uchumi umeanza kuimarika. Sasa wamarekani wana nafasi nyingi za kujiimarisha.''

Wakati huu ambapo wabunge wa Congress wangali wanabishana kuhusu maswala mengi, Obama amesema lazima wafanye uamuzi kuhusu namna ya kupunguza deni kubwa la nchi hiyo.

Alitetea mpango wake ghali wa bima ya afya ambao wabunge wa Republican waliupinga wakisema kuwa unawaunganisha wamarekani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.