Maafisa wakuu wa jeshi wafutwa kazi Sudan.K

Imebadilishwa: 23 Januari, 2013 - Saa 11:06 GMT

Serikali inalenga kufanya mageuzi katika jeshi

Sudan Kusini imekanusha madai kuwa sababu ya kuwafuta kazi maafisa 30 wakuu wa jeshi ni kuwa walikuwa wanapanga jaribio la mapinduzi.

Waziri wa mawasiliano wa nchi hiyo ameambia, BBC kuwa mageuzi hayo yanafanyika ili kuwapa nafasi vijana kushikilia nyadhifa kuu katika jeshi.

Siku ya Jumatatu, manaibu wote sita wawakuu wa jeshi, waliachishwa kazi pamoja na majenerali wengine wakuu 29.

Haya ni mageuzi makubwa kufanyika katika jeshi tangu Sudan Kusini kupatia uhuru wake mwezi Julai mwaka 2011.

Mwandishi wa BBC mjini Juba, Nyambura Wambugu anasema kuwa hakuna anayejua idadi ya wanajeshi katika jeshi la Sudan Kusini ikikisiwa kuwa kati ya wanajeshi 80,000 hadi 200,000.

Linajumuisha waliokuwa wapiganaji wa kundi la waasi, wa (SPLA) waliopigana kwa zaidi ya miaka 22.

Wanajeshi wa Sudan Kusini

Magenerali hao wametajwa kama kizingiti katika mpango wa mageuzi katika jeshi, ambalo linahitaji kuwaastaafisha baadhi ya wanajeshi kwani wanataka kusalia kuongoza vikosi vyao binafsi.

Maafisa wakuu wana muda fulani wanaoweza kuhudumu katika jeshi, na mageuzi kama haya yalihitajika kwa sababu nchi hiyo changa inajaribu kufanya mabadiliko katika jeshi.

Waziri wa mawasiliano alisema kuwa maafisa hao 35 , wamewekwa katika orodha ya maafisa wa akiba hadi malipo yao ya uzeeni yatakapotolewa.

''Hatua hii inapaswa kuwatia motisha wanajeshi badala ya kuwafanya kuwa na wasiwasi,'' alisema waziri wa habari, Benjamin Marial, na kupuuzilia mbali uhusiano wowote wa mageuzi hayo na taarifa za hivi karibuni za msukosuko wa kisiasa.

"ilikuwa fununu tu, sidhani kama kulikuwa na njama ya jaribio lolote la mapinduzi, na tunavyoongea hii leo hakuna mtu aliyekamatwa au kutuhumiwa kwa kujaribu kufanya mapinduzi,'' aliongeza bwana Benjamin.

''Wasiwasi wa usalama kwa serikali unatokana na makundi machache ya wapiganaji, ambayo yalichukua silaha tangu Sudan Kusini kujipatia uhuru kutoka kwa Sudan.'' alisema waziri huyo

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.