Wapinga kuharamishwa Miraa Uingereza

Imebadilishwa: 24 Januari, 2013 - Saa 08:45 GMT

Miraa imepigwa marufuku nchini Marekani na katika baadhi ya nchi za Ulaya

Baraza la serikali la ushauri kuhusu madawa ya kulevya, limekataa wito wa serikali kupiga marufuku Miraa au Khat.

Baraza hilo kuhusu utumiaji mbaya wa madawa ya kulvya, linasema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa miraa inasabbisha athari za kiafya.

Miraa hutumiwa sana na watu wa jamii ya wasomali, Yemeni na wa Ethiopia na imepigwa marufuku nchini Marekani, katika baadhi ya nchi za Ulaya na Netherlands.

Wizara ya mambo ya ndani ndiyo ilipendekeza kufanywa kwa uchunguzi huo.

Baraza hilo lilisema kuwa hakuna ushaidi kuonyesha kuwa Miraa ambayo ina kemikali 'cathinone 'inayochangamsha ,ilihusishwa na visa vya uhalifu wa kupangwa.

Lilisema kuwa khat, ambayo inatafunwa na wengi ili kujichangamsha ingawa athari hiyo sio kubwa ikilinganishwa na madawa mengine ya kulevya kama Amphetamine".

Elimu ya kuzuia matumizi

Makundi ya jamii ya kisomali, yaliambia baraza hilo nchini Uingereza kuwa , utafunaji wa Khat ni tatizo kubwa la kijamii

Na nchini Yemen pia watu hutumia sana Miraa

Wanaharakati walisema kuwa mmea huo unasababisha matatizo ya kiafya pamoja na kuchangia kuvunjika kwa familia.

Mmea huo hata hivyo, pia una athari zake kubwa ambazo hujitokeza baada ya matumizi ikiwemo shinikizo la mawazo, ndoto mbaya na mengineyo, ingawa haya yote sio thibitisho kuwa watu wanaweza kuwa waraibu.

Lakini mwenyekiti wa baraza hilo, Profesa Les Iversen alisema kuwa waligundua kuwa hakuna matatizo yoyote ya kiafya yanahusishwa na utumiaji wa miraa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.