Nyumba binafsi ya Zuma haina neno

Imebadilishwa: 27 Januari, 2013 - Saa 16:21 GMT
Rais Jacob Zuma

Uchunguzi uliofanywa na serikali ya Afrika Kusini haukugundua ushahidi wowote kuwa fedha za taifa zilitumiwa kujenga nyumba binafsi ya Rais Jacob Zuma - swala ambalo limezusha utata kwa miezi kadha.

Lakini Waziri wa Ujenzi, Thembalani Thulas Nxesi, aliwaambia waandishi wa habari kwamba zaidi ya dola milioni-7 za serikali zilitumiwa kuimarisha ulinzi kwenye nyumba hiyo ilioko Nkandla.

Kati ya kazi hiyo ilikuwa kujenga pahala pa helikopta kutua, zahanati na nyumba za kuishi walinzi wa rais.

Uchunguzi huo uliamua kuwa Rais Zuma hakuwa na kauli katika mipango hiyo ya usalama.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.