Mahasimu wa kisiasa wakutana Misri

Image caption Polisi wa kupambana na ghasia nchini Misri walikuwa na wakati mgumu kutuliza hali

Uongozi mkuu wa madhehebu ya Sunni nchini Misri,Al Azhar, umewakutanisha wanasiasa mahasimu kwa lengo la kujaribu kutuliza hali ya taharuki iliyotanda nchini humo.

Wanachama wa chama tawala cha Muslim Brotherhood chake Rais Mohammed Morsi, walifanya mazungumzo yao ya kwanza ya ana kwa ana tangu kuzuka kwa vurugu la kisiasa wiki jana .

Wito uliotolewa hapo awali na rais Morsi wa kufanyika mkutano wa kitaifa,ulikataliwa na upinzani.

Walisema kuwa walitaka ajitolee mwanzo katika kuhakikisha demokrasia inakuzwa nchini humo.

Zaidi ya watu hamsini wamefariki katika ghasia tangu zianze wiki moja iliyopita.