Rajoy adai hakupata pesa zisokuwa halali

Waziri Mkuu wa Uspania, Mariano Rajoy, amekanusha vikali tuhuma kwamba alipokea malipo yasiyo rasmi kutoka mfuko wa siri.

Akihutubia kikao cha dharura cha chama chake cha Popular Party, PP, Bwana Rajoy alisema "sikuwahi kupata pesa zisokuwa halali", na aliahidi kuchapisha orodha ya pato lake.

Siku ya Alhamisi, gazeti la El Pais lilichapisha nyaraka ambazo lilisema ni akaunti za siri za chama cha PP.

Nyengine zilikuwa na jina la Bwana Rajoy.