Jeshi la Ufaransa lalenga ngome za waasi

Image caption Ndege za jeshi la Ufaransa zimekuwa zikishambulia ngome za wapiganaji kwa lengo la kuziba maeneo wanayotumia kusafirishia silaha zao

UfaNdege za kijeshi za Ufaransa, zimeshambulia kwa mabomu ngome za wapiganaji na maghala yao ya silaha katika maeneo ya vijijini ili kujaribu kukata njia wanazopitishia silaha zao.

Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa, Laurent Fabius, waasi hao hawatweza kuendelea kupigana bila kupata chakula na silaha wanazohitaji.

Ndege 30 za kijeshi, zilifanya mashambulizi siku ya Jumapili, latika eneo la Tessalit huku kukiwa na hofu, kuwa wapiganaji hao huenda wakajipanga upya

Mashirika ya kutoa misaada yanasema kuwa bei ya chakula na mafuta imepanda sana huku baadhi ya wafanya iashara wakitoroka kwa hofu ya kushambuliwa.

Mkutano wa Kidal

Bwana Fabius alisema kuwa mashambulizi yaliyofanywa Jumapili, yalinuia kushambulia ngome za wapiganaji hao pamoja na vituo vya mafuta.

Image caption Askari wa Ufaransa nchini Mali

Alisema :''Ukitazama ramani, wameweza kujificha katika meeno ya Kaskazini. Lakini wanaweza kusalia huko kwa muda mrefu, ikiwa wana njia ya kupata bidhaa. Kwa hivyo, jeshi linajaribu kuziba kabisa njia za wao kupitishia bidhaa hizi.''

Lakini bwana Fabius hangeweza kusema ikiwa mashambulizi ya angani yananuia kuandaa majeshi kupigania ardhini.

Jeshi la Ufaransa, lilianza kusaidia jeshi la Mali kupambana na wapiganaji nchini Mali tarehe 11 January wakati wapiganaji wa kiisilamu walipoanza kuelekea Kusini mwa nchi na kutishia mji mkuu Bamako.

Tangu hapo, wapiganaji hao wamefurushwa kutoka maeneo ya raia Kaskazini na Mashariki mwa nchi.

Mji wa Kidal unasalia kuwa mji wa pekee muhimu ambao wanajeshi wa Ufaransa wangali kuukomboa kikamilifu.

Image caption Wapiganaji wa Kiislam nchini Mali

Mwandishi wa BBC nchini Mali amesema mashambulio hayo yamelenga maeneo ya milimani kaskazini mwa mji wa Kidal, ambako waasi hao wanadaiwa kujificha. Majeshi ya Ufaransa yamekuwa yakijaribu kuutwaa mji huo baada ya kuuteka uwanja wa ndege wa mji huo Jumatano.

Waasi wa kikundi cha Tuareg, ambao walikuwa wameudhibiti mji huo, wanaweza kuuachia kwa njia ya mazungumzo.

Askari wa Ufaransa wameudhibiti uwanja wa ndege wa Kidal.

Mashambulio hayo yanafuatia ziara ya Rais Francois Hollande wa Ufaransa nchini Mali Jumamosi.

Rais Hollande amesema majeshi yake yataendelea kuwepo nchini Mali hadi pale majeshi ya Afrika yatakapopelekwa kuilinda nchi hiyo.