Sheria ya ndoa za jinsia moja Uingereza

Image caption Sheria hii pia inaungwa mkono na upinzani

Wabunge nchini Uingereza baadaye leo wanatarajiwa kupigia kura mswaada unaruhusu ndoa za jinsia moja.

Hatua hii inaungwa mkono sana na waziri mkuu David Cameron lakini inapingwa vikali na wanacahama wa chama chake cha Conservative

Akikabiliwa na tisho la mgawanyiko chamani, chama cha Cameron, mawaziri watatu wakuu wa chama hicho, wameandika barua ya pamoja kutetea ndoa za jinsia moja.

Katika barua yao, wanahoji ikiwa ni swa kuwanyima watu haki yao ya kuoana eti kwa sababu ni wapenzi wa jinsia moja.

Sheria inatarajiwa kupitishwa kwa sababu inaungwa mkono na mwanchama wa serikali ya muungano chama cha waliberali pamoaj na kuungwa mkono na chama pinzani cha Labour.