Jela miaka 6 kwa kupokea hongo Kenya

Image caption Wapiga kura wakijisaji

Wakenya watakaopokea rushwa kutoka kwa wanasiasa ili kuwapigia kura wakati wa uchaguzi mkuu mwezi Machi huenda wakajipata matatani.

Kulingana na nakala ya sheria zilizotolewa na tume huru ya uchaguzi na mipaka , mtu yeyote atakayepokea pesa au chakula ili kumuunga mkono mgombea fulani, atakuwa anakiuka sheria za tume hiyo.

Pia mpiga kura atakuwa anakiuka sheria kwa kupokea chakula , kinywaji , pesa au vyeti kwa lengo la kushawishiwa kumpigia kura mgombea fulani, huenda akakamatwa.

Kulingana na nakala ya sheria za tume hiyo kuhusu uchaguz, maafisa maalum wa polisi watatateuliwa kutoa usalama wakati wa uchaguzi mkuu mwezi Machi.

Pia nakala hiyo inaelezea kuwa mgombea yopyte atakayetumia rasilimali za serikali kuwalazimisha wapiga kura kuwaunga wagombea fulani au chama fulani cha kisiasa.

Washukiwa wa vitendo hivyo watafikishwa mahakamani huku mkuu wa polisi akisema kesi kama hizo zitachukua miaka mitatu kabla ya hukumu kutolewa.

Yeyote atakayepatikana na hatia huenda akafungwa jela miaka sita au kutozwa faini ya shilingi milioni moja pesa za Kenya. Nchini Kenya ni jambo la kawaida kwa wanasiasa kuwashawishi wapiga kura kwa pesa au chakula ili waweze kuwapigia kura.