Misururu ya mashambulizi ya mabomu Iraq

Kumetokea misururu ya milipuko katika maeneo yenye washia wengi, nchini Iraq ambayo imewaua takriban watu 26 na kuwajeruhi wengine 85.

Katika mji mkuu Baghdad, bomu lililokuwa limetegwa ndani ya boxi, lililipuka katika soko la wanyama eneo la Kazimiya.

Dakika chache baadaye, gari liliokuwa limeegezwa pia likalipuka.

Mjini Shomali, Kusini mwa Baghdad, mabomu yaliyokuwa yametegwa ndani ya magari mawili yalilipuka.

La kwanza likilipuka katika kituo cha basi na lengine katika soko rasmi.

Hali ya wasiwasi imekuwa ikiongezeka kati ya madhehebu ya Sunni na Shia.