Shambulizi la kujitoa mhanga Mali

Image caption Mwanajeshi mmoja amejeruhiwa katika shambulizi hilo la kwanza la aina yake

Jesh la Mali linasema kuwa mashambulizi wa kujitoa mhanga amejilipua karibu na kituo cha ukaguzi cha polisi nje ya mji wa wa Gao, Kaskazini mwa Mali.

Mwanajeshi mmoja ameripotiwa kujeruhiwa katika shambulio hilo la kwanza la aina yake nchini Mali.

Wanajeshi wa Ufaransa wamekuwa wakipambana na wapiganaji wa kiisilamu karibu na mji wa Gao, ambao hadi haivi karibuni ulikuwa ngome ya waasi.

Hili ni shambulizi la kwanza la kujitoa mhanga tangu wanajeshi wa Ufaransa kuingilia kati mzozo wa Mali mwezi jana, Wamefanikiwa kuwafurusha wapiganaji hao kutoka katika miji waliyokuwa wameiteka Kaskazini mwa nchi.

Pia kumekuwa na makabiliano makali mjini Bamako, kati ya jeshi la Ufaransa na wanjeshi wanaounga mkono rais wa zamani, Amadou Toumani Toure, aliyeng'olewa mamlakani mwaka jana.