Mibuni ya Amerika Kusini yaugua

Guatemala ni nchi ya tatu ya Amerika Kusini kutangaza hali ya dharura kwa sababu ya kusambaa kwa uharibifu wa mibuni (kahawa) kutokana na maradhi yaitwayo "coffee rust", kutu ya mibuni.

Buni ni zao kubwa kabisa la eneo hilo linalouzwa nchi za nje.

Rais Otto Molina Perez alisema asili-mia-70 ya kahawa ya Guatemala sasa imeathirika; na ametoa amri serikali itoe zaidi ya dola milioni-10, kuwasaidia wakulima wadogo wadogo 60,000 kupambana na ugonjwa huo uliokaa kama uyoga.

Honduras na Costa Rica zimeshatangaza hali ya hatari kwa sababu ya "coffee rust" na El Salvador na Panama nazo piya zimeathirika.

Wataalamu wanasema ugonjwa huo wa mibuni umezidi kutapakaa kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa.