Madkatari wa Korea wauwawa Nigeria

Polisi nchini Nigeria wanasema madaktari watatu kutoka Korea Kusini wameuwawa kwenye shambulio kaskazini-mashariki mwa nchi.

Mmoja wao alikatwa kichwa.

Madaktari hao walishambuliwa ndani ya fleti yao katika mji wa Potiskum ambako inaarifiwa wakifanya kazi katika hospitali kuu.

Hakuna aliyedai kuhusika na mauaji hayo, lakini wapiganaji wa kundi la Kiislamu la Boko Haram wameuwa mamia ya watu kaskazini mwa Nigeria katika miaka mine iliyopita.