Tahadhari kwa wanawake wanaovuta sigara

Wataalamu wa afya wanasema kuwa wanawake barani Ulaya wanafariki zaidi kutokana na saratani ya mapafu kuliko saratani ya matiti.

Wanaelezea kuwa saratani ya mapafu ndio imekuwa sasa saratani nambari moja ambayo inasababisha vifo miongoni mwa wanawake.

Hali hii tayari inashuhidiwa nchini Uingereza na Poland.

Kulingana na watafiti, hii ni ishara ya idadi kubwa ya wanawake wanaovuta sigara hali iliyoanza kujitokeza kuanzia mapema miaka ya tisini na sabaini.

Idadi ya vifo vinavyotokana na saratani ya mapafu, vitaendelea kuongezeka katika miaka ijayo, lakini sasa kwa sababu ya vijana wa kike wasiovutiwa na kuvuta sigara na ambao idadi yao sio kubwa sana , huenda vifo hivyo vikapungua.

Mwaka 2013, takriban wanawake 82,640 barani Ulaya watafariki kutokana na saratani ya mapafu ikilinganishwa na wanawake 88,886 watakaofariki kutokana na saratani ya matiti.

Wanatarajiwa kuwa vifo vinvyotokana na saratani ya mapafu kupungua mwaka 2020 au 2025 kwa sababu angalu vijana wa kiike hawavuti sana sigara.

Lakini ifikapo mwaka 2015, wanawake wengi watafariki kutokana na saratani ya mapafu kuliko saratani ya matiti, kulingana na mtaalamu wa afya ya wanawake, Profesa Carlo La Vecchia .

Takwimu zinaonyesha kuwa ingawa watu wengi zaidi wanaugua saratani, kwa sababu wanaishi muda mrefu zaidi, ni watu wachache sana wanafariki kutokana na saratani.

Licha ya kupungua kwa idadi ya watu wanaofariki kutokana na saratani barani humo, idadi ya wanawakewanaofariki kutokana na saratani ya mapafu inaongezeka katika nchi zote za Ulaya.

Profesa La Vecchia,wa chuo kikuu cha Milan, Italy, anasema kuwa hali hii inaleta wasiwasi kwa sababu hakuna dalili kuwa ugonjwa huo unapungua.

Uvutaji sigara pamoja na ugonjwa wa sukari ndio vinachangia kuongezeka kwa ugonjwa huu. Lakini wataalamu wanasema bado hawajui nini kinasababisha sehemu kubwa ya saratani hiyo.

Wataalamu wanasema kuna umuhimu wa wanawake kuwacha kuvuta sigara