Ahukumiwa miaka 21 gerezani Rwanda

Image caption Maelfu ya watu wa kabila la Watutsi pamoja na wahutu waliuawa mwaka 1994

Mahakama moja nchini Rwanda imemhukumu mwanamume mmoja raia wa Rwanda miaka ishirini na moja gerezani kwa kuhusika katika mauji ya kimbari nyumbani Rwamba karibu miongo miwili iliyopita.

Mahakama hiyo imesema Sadi Bugingo alihusika na mauaji ya kati ya watu elfu moja na elfu mbili.

Hakushtakiwa kwa kuwaua moja kwa moja wahanga hao lakini hakimu amesema alihakikisha kwamba amri ya kuwaua ilitekelezwa.

Wakati wa kesi hiyo Bugingo ambaye ameishi Norway kwa zaidi ya miaka kumi alikana kuhusika kwanjia yoyote katika mauaji ya kiais ya Wanyarwanda laki nane.