Mkenya apinga waangalizi wa Ulaya

Image caption Waangalizi wanapingwa kwa kuepndelea upande mmoja kwenye uchaguzi

Mpiga Kura mmoja amekwenda mahakamani kuzuia waangalizi wa uchaguzi kutoka Muungano wa Ulaya kuweza kuingia nchini humo kwa lengo hilo wakisema kuwa wanapendelea baadhi ya wagombea.

Katika kesi iliyowasilishwa mahakamani siku ya Jumatano na Samson Ojiayo, anataka mahakama kuzuia waangalizi hao kwa Misingi kuwa wanapandelea upande mmoja , huku nchi zao tayari zikiwa ziomeonyesha kuwaonya wakenya dhidi ya kumpigia kura mgombea Uhuru Kenyatta.

Hata hivyo nchi hizo hazikulisema hilo wazi bali waliwaonya wakenya kujua athari za kuwachagua baadhi wa wagombea wa urais.

Balozi wa Marekani kuhusu maswala ya Afrika Jonny Carson, wiki jana aliwaambia wakenya kufahamu athari za kuchagua baadhi ya wagombea waliojitokeza kuwania urais katika uchaguzi wa Machi tarehe 4.

Mahakama ilifahamishwa kuwa waangalizi hao tayari wameelezea kutompenda Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake, William Ruto , kwa kutishia kwa ikiwa wawili hao watashinda uchaguzi huo , wakenya wajiandae kwa athari zake.

Kwa hivyo mtu aliyewasilisha kesi hiyo aliitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka,IEBC, kubatilisha idhini ambayo tayari imetolewa kwa waaNgalizi hao kutoka Marekani, Uingereza na Muungano wa Ulaya ambao tayari wamewasili nchini humo.

Wanapingwa zaidi kwa kupendelea upande mmoja na ikiwa ni hivyo watakuwa wanahujumu misingi ya uhuru na demkokrasia ya Kenya.

Wakili aliyekuwa anamwakilisha mlalamishi alisema kuwa waangalizi hao tayari wamependelea upande mmoja na hivyo wanapaswa kuachia jukumu lao.

''Hizi nchi pamoja na waangalizi hao, tayari wameonyesha uchokozi kwa uchaguzi wa kidemokrais utakaofanyika Kenya, kwa kusema kuwa ikiwa Uhuru na Ruto watachaguliwa,wakenya wajiandae kwa athari kwani hawatajihusisha sana na nchi hiyo,'' alisema wakili huyo

"na kwa hivyo ni muhimu kwa tume ya uchaguzi kuwapokonya vibali vya kushuhudia uchaguzi.''

Jaji Eric Ogolla, anayesikiliza kesi hiyo atatoa uamuzi Februari tarehe 18