Shekhe maarufu wa Puntland azikwa

Wajumbe kutoka sehemu zote za Somalia wanahudhuria mazishi ya shekhe maarufu aliyeuliwa Puntland Ijumaa.

Sheikh Abdul Kadir Nur Farah alipigwa risasi na mtu mmoja aliyekuwa na bunduki katika mji wa Garowe, mji mkuu wa Puntland.

Mazishi yanafanywa mjini humo.

Hakuna kundi lilodai kuhusika na mauaji hayo lakini wakuu wanamhoji mshambuliaji na wanashuku kuwa ana uhusiano na wapiganaji wa Kiislamu wa Al-Shabab.

Wadadisi wanasema shekhe huyo amekuwa akiwalaumu Al-Shabab bila ya kificho.