UN yaonya Kenya isifanye ghasia

Jumuia ya kimataifa itaingilia kati nchini Kenya iwapo ghasia zitazuka kabla au baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 4 March, endapo serikali haiwezi kudhibti hali.

Gazeti la Kenya la The East African limemnukuu mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa wa kuzuwia mauaji ya kimbari, Adama Dieng, akisema mjini Nairobi kwamba ni wajibu wa serikali ya Kenya kuhakikisha usalama wa wananchi wake kwa kuzuwia ghasia.

Bwana Dieng alisema baada ya ghasia za miaka ya '90 na baada ya uchaguzi mwaka wa 2008, jumuia ya kimataifa itafanya iwezalo kuzuwia hayo yasitokee tena.

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa alisema wanaweza kuingilia kati kwa vikwazo na kuzidisha uwezo wa serikali kupambana na ghasia.

Hatua ya tatu ni kuingilia kijeshi.