Mtafaruku wazuwia wawekezaji Libya

Mkuu wa bunge la taifa la Libya ametoa wito kufanywe juhudi zaidi kupambana na mtafaruku na rushwa katika jamii ya Libya.

Katika hotuba aliyotoa mjini Benghazi kuadhimisha mwaka wa pili tangu kuanza harakati zilizompindua Kanali Gaddafi, Mohamed Al-Megaryef alisisitiza kwamba mapatano yanahitajika.

Alisema dini zote zinahitaji kutendewa haki na alionya kuwa ukosefu wa utulivu unazuwia uwekezaji.

Walibya wengi wamekuwa wakisherehekea siku hiyo mwisho wa juma zima.