Wahisani wamuaga Oscar Pistorius

"Mimi ndio risasi katika chemba" ndiyo maandishi ya tangazo la kibiashara la kamapuni ya bidhaa za michezo ya Nike ikimuonyesha bingwa wa michezo ya Olimpiki Oscar Pistorius.

Huku mwanamichezo huyo akikabiliwa na kesi ya mauaji ya mchumba wake Reeva Steenkamp, ambayo viongozi wa mashtaka wanasema ni ya kupangwa, wahisani wake walilazimika kufanya mikutano ya dharura.

Kampuni ya Nike ilifutilia mbali tangazo hilo la biashara huku athari za kutumia wanariadha kutangaza bidhaa za makampuni zikipigwa darubini kwa mara nyingine.

Pistorius, ambaye amekanusha vikali mauaji hayo, anasemekana kujipatia mamilioni katika matangazo ya biashara ya makampuni ya Nike, BT, Thierry Mugler, Oakley na Ossur,kampuni moja nchini Icelandi ambayo hutengeza miguu ya vyuma aliyokuwa anatumia mwanariadaha huyo.

Lakini kama ilivyodunia rangi rangile kwenye michezo, mkimbiaji wa vyuma kama anavyojulikana, huenda akapoteza kila ya matangazo hayo ambayo yalikuwa yanamletea mamilioni ya pauni hata ikiwa hatapatikana na hatia.

Ilipoulizwa ikiwa inatafakai kuondoa matangazo , ya Pistorius, ambayo yanaaminika kuwa na thamani ya dola milioni mbili, msemaji wa kampuni hiyo alisema bado wanatazama hali itakavyokuwa kwani ni jambo linalohusisha polisi.

Mhisani mwingine wa Pistorius, M-Net Movies, ambayo ni runinga ya kulipia Afrika Kusini , ililazimika kuodoa matangzo yake ya kibisahara ambayo Oscar alihusika nayo.

Kupitia kwa Twitter, M-Net ilitoa rambi rambi zake kwa familia ya marehemu na kasha ikasema kuwa haina budi ila kuondoa matangazo yake ya Oscar kwenye televisheni yake mara moja.

'Bidhaa mbaya'

John Taylor, mkurugenzi wa kampuni inayotumia wanamichezo katika matangazo yao ya kibiashara, aliambia BBC kuwa "hata kama pistorius hatapatikana na hatia, sifa yake imeharibika. Kamapuni yanapaswa kuchukua hatua za haraka kujitenga naye , hayawezi kusubiri hadi kesi itakaposikilizwa."

Image caption Mchumba wake Osacr , Reever

"Sio kama panya kutoroka meli inayozama, kwa swala hili inaonekana ni hatua muhimu itakayochukuliwa, alisema msemaji huyo," alisema Taylor.

Naye Nigel Currie, mkurugenzi wa kampuni ya matangazo ya biashara katika michezo, Brand Rapport, anakubaliana na hilo akisema kuwa hili ni tofauti kabisa ikilinganishwa na yale aliyokumbwa nayo Tiger Woods na Lance Armstrong, kesi hii inahusu maisha ya mtu. Hakuna atakavyoweza kutokamana na jambo hili.

Lakini hakuna hata mhisani wake mmoja amevunja uhusiano naye na nyingi ya kampuni hizo zimekimya hata sasa.

Kampuni ya mitindo Thierry Mugler,iliyomteua Pistorius kuwa sura ya mafuta yake ya wanaume, mwaka 2011, ilisema kuwa hawana tamko lolote kuhusiana na kashfa hii na kusema uamuzi hauwezi kuchukuliwa kwa sasa.

Kampuni ya Nike huwatumia wanamichezo wanaoweza kuziweka bidhaa zake katika hadhi ya juu kabisa

Pistorius alikuwa na sifa ya kung'ang'ana ili kushinda , ari ya ushindi aliweza kufanikiwa licha ya kuwa mlemavu hali iliyomfanya kuwa mchezaji mzuri wa kutumiwa kutangaza bidhaa za makapuni ya vitu vya michezo.

Lakini kufuatia tukio la wiki jana, makampuni mengi sasa huenda yakatafakari mara mbili ikiwa yataendelea kumtumia Oscar kutangza bidhaa zao. Na sasa pia huenda wakawa makini sana na wachezaji wanaowatumia.

Katika hii dunia ya pesa na michezo, huenda akajipata ametupiliwa mbali ikiwa ana hatia au la.