Ushindani mkali kati ya Uhuru na Raila

Wagombea wa urais Waziri mkuu Raila Odinga na naibu wake Uhuru Kenyatta wanakaribiana katika kura za maoni zilizofanywa na makamapuni matatu.

Kulingana na utafiti huo, yuliofanywa kati ya tarehe 14 na 17 mwezi huu, Odinga yuko mbele huku Kenyatta akimfuata wakati mgombea mwengine Musalia Mudavadi akishikilia nafasi ya tatu.

Kulingana na utafiti wa makamapuni ya Consumer Insight, Strategic Research and PR na Infotrak, unaonyesha kuwa mmoja wawagombea hao atapigiwa kura na nusu ya watu milioni 14.3 waliosajiliwa kama wapiga kura.

Kulingana nautafiti wa kampuni ya Consumer Insight, bwana Odinga wa muungano wa CORD, atapata asilimia 45 ya kura.

Bwana Kenyatta wa muungano wa Jubilee atapata asilimia 43 ya kura wakati Mudavadi atapata asilimia tano.

Mgombea wa muungano wa Egale, Peter Kenneth atapata asilimia 3 wakati mwanamke pekee kwenye kinyang'anyiro hicho Martha Karua atapata asilimai moja.