Wakenya waomba uchaguzi salama

Bendera ya Kenya. Kenya yaamua uchaguzi

Mamia ya Wakenya wamehudhuria mkusanyiko wa mwisho wa sala mjini Nairobi, kuomba uchaguzi mkuu wa juma lijalo uwe wa salama.

Mhadhara huo wa ibada umefanywa baada ya polisi kusema kuwa vipeperushi vinavochochea fujo vilisambazwa katika baadhi ya maeneo.

Wagombea kadha wa urais walihudhuria mhadhara wa leo, pamoja na Naibu Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta.

Anakabili mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu kuhusu ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa Kenya miaka mitano iliyopita ambazo ziliuwa watu zaidi ya elfu moja.