Hali ya sintofahamu Italia baada ya uchaguzi

Raia wa Italia wanakabiliwa na hali ngumu ya kisiasa baada ya matokeo ya uchaguzi kuonyesha kuwa hakuna aliyepata ushindi wa moja kwa moja.

Mrengo wa kushoto unaelekea kupata ushindi mdogo zaidi katika bunge la chini lakini mrengo wa kulia unaoongozwa na aliyekuwa waziri mkuu Silvio Berlusconi atadhibiti bunge la Senate.

Mwanasarakasi Beppe Grillo ambaye alipata zaidi ya asili mia ishirini katika mabunge yote mawili amesema kuwa hataungana na upande wowote kisiasa.

Kiongozi wa mrengo wa kushoto, Pier Luigi Bersani ametaja hali hiyo kuwa telezi mno.