Mpango wa amani walemazwa Ivory Coast

Image caption Jeshi la Ivory Coast linatuhumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu

Ripoti kutoka katika shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema kuwa mpango wa amani na maridhiano nchini Ivory Coast umelemazwa na visa vya ukiukaji wa haki za binadamu vinavyotekelezwa na wanajeshi.

Zaidi ya miezi sita shirika hilo limeandaa ripoti kuhusu mateso, mauaji ya kiholela na kukamatwa kinyume cha sheria na jeshi la nchi lililobuniwa na rais Allassane Ouattara.

Jeshi hilo lilitakiwa kuchanganywa na lile la mtangulizi wa , Laurent Gbagbo, baada ya ghasia ya baada ya uchaguzi ya 2010.

Duru zinasema kuwa jeshi pamoja na wapiganaji wanafanya uhalifu bila kujali sheria.